PUNGUZA KILO 9 NDANI YA WIKI NNE!!!!

Breakfast, Lunch na Dinner kwa shilingi 10,000 tu kwa siku! piga 0715808038 kujiunga.

Wednesday, March 7, 2012

Lazima kujiandaa kisaikolojia kupungua uzito

Uamuzi wa kupunguza uzito unahitaji kuhusisha juhudi za akili na mwili. Kiakili unahitaji kujiandaa kwa staili mpya ya maisha ambayo ni muhimu sana katika kupunguza mwili.

kuanza diet au staili mpya ya maisha inahitaji maandalizi. sio tu kujiandaa kwa mazoezi na kua na vyakula vinavyohitajika karibu, ila unahitaji kujiandaa kiakili/ kisakolojia kupunguza uzito au mwili wako. Fikiria jinsi mambo yanavyokua tofauti ukiwa  kwenye diet na jinsi maisha yako yatakavyokua pindi utakapofikia uzito unaotaka.


Kufanikiwa kupungua mwili kunatokana na utashi na kuwa na uwezo wa kufuata mpango wa chakula. Utashi huo unatokana na jinsi unavyochukulia zoezi zima la kupungua mwili na kufuata diet. Vuta taswira ya utakavyokua baada ya kufikia uzito unaolenga. Amini kwamba unaweza kufikia malengo ya uzito wako na jitoe kwa moyo kufanya hilo kutokea.


Hatua ya kwanza; Chukua muda wa kutathmini kwa nini wewe ni mnene. Baini sababu zilizopelekea kutokea kwa matatizo yako uzito.
Hatua ya pili; Fikiria kwa picha utakavyokuwa baada ya kupungua uzito unaotaka kama motisha kwa diet yako. Fikiria jinsi muonekano wako utakavyo kua baada ya kupungua saizi kadhaa. usitizame tu kwa urahisi jinsi utakavyoonekana kwa nje, ila fikiria pia mabadiliko utayopata ndani yako, jinsi utakua una jiamini na kujiona mzuri na wa kuvutia.
Hatua ya 3;  Tunga orodha ya malengo yako yote ya muda mrefu na muda mfupi kwa ajili ya staili ya mlo wako.
Hatua ya nne; Pima kilo/ uzito wako kila wiki au mara moja kwa wiki mbili kujua mabadiliko ya uzito wako. 
Hatua ya tano; Tafuta mpangilio mzuri wa kula au diet utakao kufaa. Kisha anza mazoezi na diet yako kwa moyo.

No comments:

Post a Comment