PUNGUZA KILO 9 NDANI YA WIKI NNE!!!!

Breakfast, Lunch na Dinner kwa shilingi 10,000 tu kwa siku! piga 0715808038 kujiunga.

Tuesday, April 10, 2012


KWA ujumla wake, karoti ni mboga yenye kiasi kingi cha Vitamin A. Mbali ya vitamini hiyo, karoti ina virutubisho vingine muhimu vyenye uwezo wa kuzuia magonjwa hatari, kama vile saratani, moyo na mengine mengi na kumbuka kwamba; ‘kinga ni bora kuliko tiba’.
Sifa pekee na kubwa kuhusu karoti inayojulikana na watu wengi, ni uwezo wake wa kuimarisha nuru ya macho na uwezo wa kuona, hususan wakati wa usiku. Katika makala ya leo nitakufahamisha faida nyingine za mboga hii rahisi, inayopatikana kwa wingi, mijini na vijijini. Ukiielewa vizuri, itaokoa maisha yako.

VIRUTUBISHO VYA KAROTI
Kwa mujibu wa tafiti kadhaa zilizofanywa, imethibitika kuwa karoti ina kiwango kikubwa cha virutubisho jamii ya ‘carotenoids’ ambavyo husaidia sana kuupa mwili uwezo wake wa asili wa kupambana na maradhi yanayojitokeza mwilini.
Katika utafiti huo, imeelezwa kuwa ulaji wa karoti, hata kwa kiasi cha karoti moja tu kwa siku, kinampunguzia mlaji uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa saratani ya matiti kwa asilimia 20.
Aidha, imeainishwa zaidi kuwa, mlaji wa karoti moja kwa siku, atakuwa pia anajiepusha na kupatwa na saratani za aina nyingine kwa asilimia 50. Saratani hizo zimetajwa kuwa ni saratani ya kibofu cha mkojo, kizazi, utumbo, mapafu na saratani ya koo.
Katika utafiti wa hivi karibuni wa Taasisi ya Saratani ya Taifa nchini Marekani (National Cancer Institute), imebainika kuwa wagonjwa wengi waliogundulika na saratani ya mapafu, katika milo yao walikuwa hawatumii karoti wala vyakula vingine vyenye virutubisho jamii ya ‘carotenoids’.

KAROTI NA UGONJWA WA KISUKARI
Kama tujuavyo, ugonjwa wa sukari ni maradhi yanayowasumbua watu wengi duniani na hauna tiba. Magonjwa kama kisukari, huweza kumpata mtu kutokana na mpangilio mbaya wa vyakula anavyokula kila siku na staili ya maisha anayoishi kwa ujumla.
Mtu anaweza kujiepusha na magonjwa mengi hatari, kama kisukari, kwa kuzingatia ulaji usahihi. Kutokana na kiwango cha virutubisho mbalimbali vilivyomo kwenye karoti, mgonjwa wa kisukari anaweza kupata ahueni kwa kufanya karoti kuwa sehemu ya mlo wake wa kila siku.
Watafiti wamegundua kwamba virutubisho vilivyomo kwenye karoti, vina uwezo mkubwa wa kurekebisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo kutoa kinga au kumpa mgonjwa nafuu kubwa.

KAROTI NA MAPAFU
Kama unaishi au unafanyakazi katika mazingira yenye moshi au wewe ni mvutaji wa sigara, ulaji wa vyakula vyenye vitamin A kwa wingi kama karoti, humuepusha mvutaji na uwezekano wa kupatwa na saratani ya mapafu. Ulaji wa vyakula aina hii kwa mvuta sigara, si wa hiyari kama anataka kujiepusha na saratani ya mapafu.

JINSI YA KUCHAGUA NA KUHIFADHI KAROTI
Kwa kawaida, karoti huwa ni mzizi ulionyooka wenye rangi za kung’aa. Zipo karoti za rangi tofauti, lakini karoti bora ni ile tuliyoizoea yenye rangi ya chungwa na kwa mujibu wa utafiti, karoti yenye rangi iliyoiva sana ndiyo yenye virubisho vingi zaidi.
Karoti inaweza kudumu kwa muda mrefu ikihifadhiwa vizuri. Hifadhi karoti yako kwenye jokofu ikiwa kwenye mfuko wa plastiki ambao hauruhusu kupitisha hewa nyingine, ikihifadhiwa vyema, karoti inaweza kukaa hadi wiki mbili bila kuharibika.

Aidha, wakati wa kuhifadhi karoti yako katika jokofu, usichanganye na matunda mengine kama vile ‘peasi’, nyanya, ‘epo’ na matunda mengine ya jamii hiyo. Inaelezwa kuwa kwa matunda hayo kukaa pamoja, kunaweza kuifanya karoti kuwa chungu.
Kabla ya kuhifadhi karoti kwenye jokofu, hakikisha umekata majani yake ya juu na mizizi yake ya chini, ili kuzuia karoti kuchipua licha ya kuwa kwenye jokofu.

JINSI YA KUANDAA NA KUILA KAROTI
Osha vizuri karoti yako kwa kutumia kifaa maalumu cha kusugulia pamoja na maji safi. Wakati wa kuosha karoti, vizuri utumie maji ya kutiririka na siyo yaliyotuama. Hii inamaana kwamba osha karoti kwenye maji ya bomba au kwa kumimina na chombo, usioshee ndani ya chombo kuepuka kuondoka na vijidudu.

No comments:

Post a Comment